Amina Mollel awataka wazazi kutowaficha watoto wenye ulemavu - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 7 November 2017

Amina Mollel awataka wazazi kutowaficha watoto wenye ulemavu

Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliekuwa rika la Kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo.
Na  Woindeshizza Blog
Wazazi hususa ni jamii ya kimasai wametakiwa kuachana na zana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike na wale ambao ni walemavu  badala yake wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae
Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa akizungumza kama mgeni rasmi katika sherehe za  kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika   Kijiji cha Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha
Alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha  watoto wao kisa ni walemavu jambo ambalo linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu  kutokana na kufichwa huko
“kwakweli wazazi wanavyoficha watoto wao hususa ni walemavu  wanawanyima haki yao mfano kama mimi ningefichwa leo kweli ndugu zangu ningeweza kuwa kiongozi hivyo napenda kuwasihi wazazi wasiwafiche watoto hawa kwani wakiwapeleka shule kupata elimu itakuwa vizuri kwani pale watakapo maliza shule wanakuja kuwasaidia  “alisema Amina.
Aidha pia aliwataka wazazi hawa wa jamii ya kimasai na hata wale wa makabila mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto hao wakike nao wanahaki ya kupata elimu kwani elimu ni bure ,kuanzia  ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo ni vyema kama wazazi wakawasimamia watoto hususa ni wakike wakaenda shule
Aliongeza kwa kuwasihihi watoto wa kike kuweka kipaumbele swala la elimu kwani elimu ndio kila kitu katika maisha yao na iwapo watasoma kwa bidii wanaweza kuwa viongozi  wakubwa wa serikalini hapo baadae
Alisema kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha kusoma kisa wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza kukimbilia maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza alafu maisha watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri
“napenda kuwasihi ndugu zangu wamasai kuachana na mila za kizamani kama vile ukeketaji na kuozesha watoto wa kike mapema kwani swala hilo sio jema na limepitwa na wakati na napenda kuwataka wananchi wote hususa ni ndugu zangu wamasai kuwafichua wale wote ambao bado wanaendeleza mila za zamani kama vile ukeketaji”Alisisitiza Amina

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here