Dah Aslay sio kwa ndinga hili la kifahari aina ya BMW ‘bado nyumba ya kifahari’ - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday 8 November 2017

Dah Aslay sio kwa ndinga hili la kifahari aina ya BMW ‘bado nyumba ya kifahari’


Kweli muziki Unalipa!. Aslay ameanza kuishi maisha ya kifahari kwa ngoma zake kadhaa alizoziachia ndani ya mwaka huu baada ya kuachana na Kundi la Yamoto Band lililokuwa likisimamiwa na Mkubwa Fella.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa amenunua gari hilo kwa pesa iliyotokana na nyimbo zake kadhaa alizoziachia mwaka huu.
“Mungu ni mwema sana, kweli nimenunua BMW, ni gari ambayo nimeona ina hadhi hata nikitokea mbele ya mashabiki wa muziki wangu kuna heshima inajengeka. Kwahiyo hivi ni moja kati ya vitu ambavyo nilitamani kuwa navyo,” alisema Aslay.
Aliongeza, “Kwenye ishu ya nyumba, mimi nataka kuwa na nyumba ambayo mtu akiingia asema hii kweli ni nyumba ya kifahari, nzuri inavutia,”
Hata hivyo Aslay hakuweka wazi dharama halisi aliyotumia kununua gari hilo.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri ya wimbo ‘Natamba’ ni mmoja kati ya wasanii ambao wamepata show nyingi za ndani ya Tamasha kubwa la muziki nchini la Fiesta.
     chanzo Bongo5

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here