Uhusiano wa Wema Sepetu na Idris Sultan unaanza kutukumbusha ule wa
Chris Brown na Karrueche Tran ule wazungu wanauiita ‘off and on.’
Baada ya hivi karibuni kuzinguana tena hadi kumfanya Idris ajiondoe
Instagram hadi sasa, wawili hao wanaonesha kuanza kutafuta suluhu.
Wema amepost picha hiyo juu Instagram inayoonesha walikuwa wakiwasiliana
kutumia app ya Facetime, aliandika:That moment you realise how much u miss a special someone… Rudi
basi… hata kidogo tu
Wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya Wema
kuisusia show ya Idris, Funny Fellas kwa mara nyingine tena huku mshindi huyo
wa Big Brother akihudhuria za mpenziwe, ikiwemo Black and Tie iliyofanyika
mwezi uliopita.
Baada ya kuchoshwa na tabia ya
mpenzi wake kutompa support kwenye show zake, Idris naye aliamua kuipotezea
show ya Usiku wa Vigoma iliyoandaliwa na Sepetunga mwishoni mwa wiki – na hapo
ndipo mambo yalipoharibika.
Mashabiki wa Wema walikasirika
baada ya shemeji yao kuikwepa show hiyo na wanamshambulia Instagram. Kutokana
na kuandamwa, Idris amelazimika kuongea:
Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua
maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu
mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti
naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ?
Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?
Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show
yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because
anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa
kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal
life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out
hajaja.
“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have
respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good
reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua
this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu
mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia
TusichukulianePoa.

No comments:
Post a Comment