Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue amesema yeye ana mchango mkubwa
katika mabadiliko ya muziki wa bongofleva nchini.
Akiongea katika kipindi cha Ndoto Kubwa cha Clouds TV
Jumapili hii, Mr Blue amesema yeye ndiye msanii wa kwanza kufanya muziki akiwa
na swagga.
“Mimi baada ya kuingia kwenye
muziki kuna vitu ambavyo nilivifanya mimi kama mimi ili kuonyesha utofauti,
kuanzia kwenye kuvaa, swagga za kuimba, kutoboa masikio.
Kwa hiyo hivyo vyote
kwa wakati ule watu walikuwa wananiona huyu jamaa vipi, kumbe mimi tayari
nilikuwa nimeshaiona future, ndio maana wasanii wengi waofanya muziki kwa
swagga, utasikia ana flow kama Mr Blue, tayari tulishaacha alama huko ndiyo
maana tunaendelea kufanishwa,”
Katika hatua nyingine Blue amesema
yeye alikuwa anapenda kusoma kuliko kufanya muziki, lakini akaamua kujifunza
kufanya muziki mpaka akaweza.

No comments:
Post a Comment