Idadi ya vifo kufuatia kimbunga
Matthew nchini Haiti inakaribia watu 300, kwa mujibu wa serikali.
Katika Mji wa Jeremie asilimia 80 ya majengo yameporomoka.
Hadhi ya Kimbunga Matthew kwa mara nyingine imepandishwa hadi
ngazi ya nne, hatua ambayo ndiyo ya pili kwa ukubwa katika mgawanyo wa aina
mbali mbali za Kimbunga, huku kikielekea katika jimbo la Florida nchini
Marekani.
Maafisa wa serikali ya Haiti wametoa takwimu mpya kuhusiana na
maafa yaliyosababisha na kimbunga hicho.
Siku ya alhamisi, serikali ya nchi hiyo ilisema watu mia moja
tayari walikuwa wamepoteza maisha yao.
Kimbunga Matthew ambacho ndicho kubwa zaidi katika visiwa vya
Caribbean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada
ya kupitia Haiti na Cuba.
Wengi wa waliopoteza maisha nchini Haiti, walikuwa wakiishi
mjini na vijiji vinavyojulikana kwa shughuli za uvuvi katika maeneo ya pwani ya
kusini.
Wengi walifariki baada ya kuangukiwa na miti, taka zilizokuwa
zikisombwa au hata kusombwa na maji, baada ya mito nyingi kuvunja kingo zao.
Kimbunga hicho kiliambatana na upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi
ya hadi kilomita 280 kwa saa.
Usafiri kati ya maeneo ya kusini Magharibi na meneo
mengine nchini Haiti ulisitishwa baada ya daraja moja muhimu inayounganisha
maeneo hayo kusomba na maji.
Mashirika yasiyo ya kiserikali
yamesema kwa sasa hakuna huduma za simu na umeme na kuwa watu wanapungukiwa na
vyakula na maji safi ya kunywa.
Mratibu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya misaada ya
kibinadam amesema kuwa zaidi ya watu laki tatu na nusu wanahitaji misaada ya
kibinadamu.
No comments:
Post a Comment