Baraza la Mawaziri nchini Burundi, kwa
kauli moja limeidhinisha mswada wa kuliondoa taifa hilo kutoka kwa Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu, ICC.
Serikali ya nchi hiyo tayari imewasilisha mswada huo bungeni
ambapo unatarajiwa kujadiliwa na hatimaye kuidhinishwa.
Makamu wa rais Gaston Sindimwo amesema serikali ya Burundi
haiogopi kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa.
"Wajua, huenda tukatengwa. Lakini ni sawa mradi tu tuwe
tunajivunia uhuru wetu. Ni nchi ngapi hazijajiunga na mahakama hii? Zimetengwa?
Kuna Marekani, Urusi, Uchina na nyingine nyingi na kun ahata mataifa jirani
hapa ambayo hayajajiunga na mahakama hiyo," alisema.
"Lakini bado yameendelea kuwepo. Hatufanyi chochote kibaya.
Ni haki yetu kujitoa mahakama ya ICC. Ni uamuzi wetu; mswada sasa umewasilishwa
bungeni. Tuko tayari kwa matokeo yoyote."
Zaidi ya watu 400 wameuawa kwenye machafuko yaliyotokea tangu
rais Pierre Nkurunziza aamue kuwania urais kwa muhula wa tatu Aprili mwaka wa
2015. Wengine 200,000 wametorokea mataifa jirani wakihofia usalama wao.
Wafuasi wa serikali na wale wa upinzani pia wamekuwa wakiuawa
mara kwa mara katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Pierre Nkurunziza
ni nani?
§
Alizaliwa 1964
§
Alikuwa kiongozi wa waasi lakini baadaye akawa rais
§
Ni Mkristo
§
Alikuwa mwalimu wa michezo
§
Hupenda sana kuendesha baiskeli na kucheza kandanda
§
Ameoa na ana watoto watano
§
Babake aliuawa wakati wa vita vya kikabila mwaka 1972
No comments:
Post a Comment