Msanii Alikiba ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Aje' amefunguka na kusema kuwa yeye anaishi maisha ambayo amechagua yeye na kusema hawezi kuishi maisha kama ambavyo wasanii wengine wanaishi na kudai kuwa anapenda kuishi maisha ya kawaida na si maisha ya kisupa star.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo Alikiba amedai kuwa licha ya kupata mkataba na kampuni kubwa ya muziki ulimwenguni 'Sony Music' lakini yeye ataendelea kuishi maisha yake ya kawaida.
"Unajua mimi haya maisha nayoishi nimechagua, sipendi kuishi maisha ya kistaa kama wengine hata sasa licha ya kupata dili hili nitaendelea kuishi maisha yangu ya kawaida, ila kama ningetaka kuishi maisha ya kistaa uwezo huo nilikuwa nao hata kabla ya kusaini huu mkataba".
Mbali na hilo Alikiba amedai yeye kupata dili hili la Sony Music na mafanikio makubwa aliyopata ndani ya muda mfupi toka amerudi kwenye game anaona ni kama amepiga msamba si hatua tu.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Friday, 27 May 2016
Home
Unlabelled
Alikiba Adai Kuwa Anapenda Kuishi Maisha Ya Kawaida Na Si Maisha Ya Kisupa Staa
Alikiba Adai Kuwa Anapenda Kuishi Maisha Ya Kawaida Na Si Maisha Ya Kisupa Staa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Responsive Ads Here


No comments:
Post a Comment