Msanii mkongwe wa muziki kutoka mkoani Morogoro, Afande Sele
ambaye alikuwa mgombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi uliopita kwa tiketi ya
ACT Wazalendo amefunguka kwa kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa viongozi wa
Chama cha ACT-Wazalendo.
Rapper
huyo amesema viongozi wa chama chake hawaeleweki wapo upande gani kutokana na
kubadilisha misimamo yao kila mara.
“Chama changu cha Act-Wazalendo
bwana wakati flani hata mimi sikielewi kama ni malaika au shetani. Ni kama
kiumbe aitwae mkunga haeleweki ni samaki au nyoka zaidi tumekuwa kama popo
hatupo katika kundi la ndege au mnyama…labda hatueleweki au hatujielewi kwa
mfano wakati wa kampeni viongozi wetu walijikita kuponda wapinzani wenzetu hasa
mzee Lowasa na UKAWA na baada ya uchaguzi viongozi wetu wakampongeza Magufuli
kiasi cha kujipendekeza hadi wakampa Ilani ya chama chetu akaitumie akiwa
Ikulu. sasa ajabu leo hii tumegeuka tena kwa kiongozi mkuu kila siku anamponda
Rais Magufuli na chama chake halafu kiongozi wangu mwingine comrade mchange
yeye kila siku anamponda mzee Lowasa na ukawa yake” aliandika kupitia facebook.
Aliongeza “Katika mgogoro wa CUF unaoendelea sasa hivi
eti viongozi wote hao wa chama chetu wamejigeuza team Lipumba…sasa sielewi sisi
kama wanachama tusimamie wapi….’Nyuma ya pazia’dilidilisha…mchongo=mchongoma…ni
bora kuwa Moto au Baridi kuliko kuwa vuguvugu kwani vuguvugu ni ishara ya
unafki ambao hata maandiko yanakataza…Kweli itatuweka huru
No comments:
Post a Comment