FA imetoa adhabu kwa vilabu vya Chelsea na Tottenham - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 17 May 2016

FA imetoa adhabu kwa vilabu vya Chelsea na Tottenham

Chama cha soka nchini Uingereza FA May 16 kimetoa adhabu kwa vilabu vya Chelsea na Tottenham timu hizo zote zinatoka jiji moja la London, FA wametangaza uamuzi wa kuvipiga faini vilabu hivyo kutokana na kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
1231B4BD00000514-3593343-image-a-21_1463418250966
1231B4BD00000514-3593343-image-a-21_1463418250966
FA imetangaza kuipiga faini Chelsea ya pound 375,000 ambazo ni sawa Tsh bilioni 1 ya kitanzania, wakati klabu ya Tottenham Hotspurs imepigwa faini ya pound 225,000 ambayo ni zaidi ya Tsh milioni 700 za kitanzania, maamuzi yametokana na wachezaji wa timu hizo kufanyiana vitendo visivyo vya kinidhamu wakati wa mchezo dhidi yao.

1231928F00000514-0-image-a-1_1463417594738
1231928F00000514-0-image-a-1_1463417594738
Mechi hiyo ilichezwa Stamford Bridge iliisha kwa sare ya goli 2-2, lakini muamuzi alitoa jumla ya kadi za njano 12, hata hivyo mapema mwezi huu Mchezaji Mussa Dembele wa Tottenham alifungiwa mechi sita kutokana na kumpelekea vidole Diego Costa wa Chelsea machoni kwa makusudi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here