Mahusiano kati ya mwanamitindo, Daphne Joy (29) na mwanamuziki wa Msrekani Jason Derulo (26) yamevunjika.

Daphne Joy na Derulo wamedumu kwenye mahusiano kwa muda wa miezi saba pekee huku mwanzoni mwa mwaka wawili hao walionekana wakila bata pamoja nchini Mexico.
Kabla ya hapo mwanamitindo huyo [Daphne Joy] aliwahi kuwa na mahusiano na rapa 50 Cent na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja, Sire (3).
Rafiki wa karibu wa mwanamitindo huyo ameiambia TMZ kuwa Dephne ndiyo alitaka mahusiano hayo na Derulo yavunjike.

No comments:
Post a Comment