Mtoto wa marehemu, Chacha Wangwe afikishwa kortini kwa makosa ya kimtandao. - OREST NGOWI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Thursday, 12 May 2016

Mtoto wa marehemu, Chacha Wangwe afikishwa kortini kwa makosa ya kimtandao.

Responsive Ads Here
1

BOB Chacha Wangwe (24), mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii.

Akisoma kesi hiyo namba 167, Paul Kagoshi mbele ya Waliarandwe Rema, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo alisema kuwa, Bob Chacha Wangwe amefikishwa mahakamani hapo kwa kutenda kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake Facebook.

Mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo  tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya; “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad