Sioni sababu ya wasanii wa Bongo kuwa na bifu – Sugu - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 27 May 2016

Sioni sababu ya wasanii wa Bongo kuwa na bifu – Sugu

Rapper mkongwe Joseph Mbilinyi aka Sugu amesema kuwa haoni faida ya bifu wanazoziendeleza wasanii wa Bongo.
13261081_239625283079224_1295403943_n
Sugu ambaye kwa sasa video yake ya ‘Freedom’ inafanya vizuri kwenye TV na redio, ameiambia Clouds TV, kupitia kipindi cha Clouds 360 kuwa haoni faida ya wasanii kuendekeza tofauti.

“Kuna vitu ambavyo mimi sivipendi sasa hivi , team nani team nani.Kwa sababu mtu akishafanikiwa akiwa pale top hatuhitaji wawe wawili au mmoja tunataka wawe wengi ili wakishafanikiwa watatoa ajira za kutosha,” alisema Sugu.
Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini aliongeza kuwa, “Mimi Sioni kama ina faida kwa sababu zinamfanya mmoja lazima apotee. Mimi nataka wote wanyanyuke.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here