Jeneza la Muhammad Ali laswaliwa Marekani - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 10 June 2016

Jeneza la Muhammad Ali laswaliwa Marekani

Muhammad Ali
Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yamefanyika katika jimbo la Kentucky, Marekani.
Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.

Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville.
Ali
Swala hiyo inapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani.
Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu.
Maelfu
                            Mazishi yake yatafanyika Ijumaa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here