Muigizaji Amber Heard hakuweza kuripoti vitendo vya unyanyasaji nyumbani aliokuwa akifanyiwa na mume wake Johnny Depp kwasababu alitaka kulinda faragha yao, mawakili wake wamesema Jumanne hii.
Heard, aliyeigiza na Depp kwenye filamu ya mwaka 2011, “The Rum Diary,” alidai kuwa ndoa yake imekuwa ya matatizo.
Wawili hao wamedumu kwa miezi 15 kwenye ndoa. Na sasa Heard anataka talaka huku akidai kuwa May 21 mime wake hugo alimponda na simu usoni.
Heard akiingia kwenye mahakama kusikilizwa kesi yake ya talaka. Anadai Deep amekuwa akimnyanyasa kimwili na kisaikolojia
Heard aliambia mahakama kuwa amekuwa akiishi na hofu na mume wake ambaye ni mlevi ambaye amekuwa akimteka kimwili na kihisia. Muigizaji hugo wa The Pirates of the Caribbean bado hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.
Amber Heard
No comments:
Post a Comment