Rais wa Angola amteua bintiye mkuu wa mafuta - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 3 June 2016

Rais wa Angola amteua bintiye mkuu wa mafuta


Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, amemteua binti yake kuwa mkuu wa shirika la mafuta la kitaifa la Sonagol.
Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, amemteua binti yake kuwa mkuu wa shirika la mafuta la kitaifa la Sonagol.


Isabel dos Santos ndiye mwanamke tajiri zaidi barani Afrika
Rais aliwaachisha kazi wanachama wote wa bodi ya shirika hilo mnamo mwezi Aprili, mwaka huu.
Vyombo vya habari nchini vinasema kuwa Isabel dos Santos anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika shirika hilo ili kuimarisha utendakazi na faida katika shirika hilo.
Angola ni taifa la pili katika uzalishaji wa mafuta barani la Afrika.
Binti dos Santos ambaye ametambuliwa na jarida la Forbes kama mwanamke tajiri zaidi barani Afrika; tayari ameekeza katika sekta ya simiti, benki na mashirika ya mawasiliano na uchimbaji wa almasi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here