Mwanamuziki wa kufoka kutoka Marekani 50Cent alilazimika kulipa faini ya dola elfu ishirini pesa za Marekani baada ya kutumia maneno yenye matusi alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko katika kisiwa cha St Kitts and Nevis.
Fifty cent ambaye anafahamika kwa jina kamili Curtis Jackson alikuwa amepangiwa kuwa 'Mcee' katika tamasha hilo la muziki huko Caribbean lakini alipopanda jukwaani mashabiki walimsihi awape kionjo cha muziki wake.
Alipokubali 'DJ' alicheza wimbo wake mmoja na wimbo huo ulikuwa na matusi kochokocho jambo ambalo ni hatia katika kisiwa hicho kilichotawaliwa na Uingereza.
50 cent hakufahamu alikuwa amevunja sheria hadi alipofika katika uwanja wa ndege siku ya Jumapili akikusudia kuondoka.
Hata hivyo maafisa wa forodhani walimkamata na kumzuilia hadi jumatatu alipofikishwa mbele ya hakimu na kusomewa mashtaka yake.
50 cent alikiri makosa yake na kupigwa faini ya takriban dola 20,000 pesa za marekani kabla ya kuruhusiwa kuondoka.
Funzo ?
Kaa nao ujue tabia zao.
No comments:
Post a Comment