Waziri Mkuuwa Israel
benjamin Netanyahu anakamilisha ziara yake barani Afrika Alhamisi nchini
Ethiopia ambapo anatarajiwa kukutana na viongozi wa serikali na kutia saini
mikataba kadhaa ya maendeleo. Tangu kuwasili kwake barani Afrika Julai 4,
Netanyahu amezuru Uganda, Kenya na Rwanda katika kile alichokitaja kama histori
kubwa kwa Israel kurejea barani Afrika. Amekuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Israel
kuzuru Afrika katika kipindi cha miaka thelathini.
Ethiopia ilikuwa
mojawapo ya nchi za kwanza barani Afrika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na
Israel katika miaka ya sitini. Lakini uhusiano huo umeyumba yumba mara kadhaa
baada ya Ethiopia kuukatiza mara kadhaa katika historia yake.
Hii ilidhihirishwa
zaidi wakati wa vita vya Waarabu na Israel mwaka 1973 wakati Ethiopia
iliposimama pamoja na mataifa mengine ishirini ya Afrika; kukatiza uhusiano
kidiplomasia na Israel. Hata hivyo maaptanao yaliafikiwa tena katika miaka ya
1980 baada ya Israel na Misri saini mkataba wa amani mwaka 1979.
Hata hivyo, katika
mwaka 1984 Ethiopia ilipokuwa ikikabiliwa na kiangazi na migogoro ya kisiasa
wakati wa utawala wa Mengistu Haile Mariam, Israel ilihofia usalama wa maelfu
ya Wayahudi wa Ethiopia na kuwaondoa elfu saba kati yao katika safari za siri
za ndege katika kile kilijulikana kama kama Operation Moses. Shuguli hiyo
iliisababishia Ethiopia aibu kubwa huku awali ikidai kwamba walikuwa wametekwa
nyara. Miaka sita baadaye, wengine elfu kumi na nne zaidi walisafirishwa hadi
Israeli katika siku mbili tu. Sasa kuna zaidi ya Wayahudi mia moja na
thelathini elfu kutoka Ethiopia wanaoishi nchini Israeli.
Hatima ya wengine elfu
tisa ambao bado wako Ethiopia inatarajiwa kuangaziwa katika mazungumzo kati ya
serikali hizo mbili baadaye Alhamisi. Licha ya hayo, nchi hizo mbili
zinajivunia kuwa washirika wa karibu katika vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi
na kuwa na msaada wa Marekani. Ziara pia anatarajiwa kuendeleza mahusiano baina
ya nchi hasa katika maeneo ya biashara, usalama, kilimo na

No comments:
Post a Comment