Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi
Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta
hiyo.
Awali kamati ya jopo hilo
inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa
yamedukuliwa.
Vyombo vya habari Marekani vinasema
kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.
Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema
kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha
udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.
Juma lililopita mtandao wa kufichua
habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi
ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.
No comments:
Post a Comment