Wanasayansi wanakadiria setilaiti
hiyo ilifika muda mfupi ujao majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za Afrika
Mashariki.
Setilaiti hiyo inatarajiwa kudumu
kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi ilivyoumbwa.
Mawasiliano kutoka kwa chombo hicho
cha juu yalipokelewa katika maabara ya Nasa eneo la Pasadena, California kwa
shangwe.
"Vituo vyote vya Juno,
tunapokea sauti ya kufanikiwa kwa chombo Delta B," kituo cha udhibiti wa
Juno kilitangaza. "Roger Juno, karibu Jupiter."
Wanasayansi
wanatarajiwa kutumia chombo hicho kufahamu Zaidi muundo wa sayari ya Jupiter
ambayo hujulikana kwa Kiswahili kama Zohali.
Wanafikiri muundo wake kikemia unaweza kutoa ufahamu kuhusu
jinsi sayari hiyo iliundwa miaka bilioni nne unusu iliyopita.
Hakuna chombo cha anga za juu kilichowahi kufika karibu sana na
sayari hiyo kama kilivyofanya chombo cha Juno.
Miali nururishi kutoka kwa sayari hiyo huwa na uwezo wa kuharibu
vyombo vya kielektroniki visivyokingwa vyema.
Chombo vya Juno kimezingirwa na kinga ya madini ya Titanium.
Kwa sasa Juno itakuwa ikichukua siku 53 kuizunguka sayari hiyo.
Baadaye Oktoba, itaongeza kasi na kuikaribia zaidi sayari hiyo
na kuanza kutumia siku 14 kumaliza mzunguko.
Lengo kuu litakuwa kubaini iwapo kuna oksijeni katika sayari
hiyo. Hii sana itakuwa imefungamanishwa na maji, iwapo yapo.
"Kiwango cha maji katika sayari ya Jupiter kitatueleza
mengi kuhusu ni wapo sayari hiyo ilikuwa ilipoundwa mapema katika mfumo wa
jua,” anasema mmoja wa wanasayansi wanaohusika katika mradi huo Candy Hansen.
"Tunafikiri kwamba Jupiter iliundwa ikiwa pahala tofauti na
ilipo sasa."
§
Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara
300 zaidi
§
Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja
huko hudumu saa 10.
§
Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.

No comments:
Post a Comment