Msanii mkongwe wa filamu Jacob Stephan ‘JB’ amefunguka
kwa kusema kuwa ataachia filamu yake moja ya mwisho na baada ya hapo atawaachia
vijana fani hiyo.
Muigizaji huyo ambaye yupo mbioni kuachia filamu yake
mpya ‘Kalambati Lobo’, amesema baada ya filamu hiyo ataachia filamu moja na
mwisho na baada ya hapo atapumzika.
“Nimekuwa nikipokea simu nyingi na meseji kutoka kwa wapenzi
wangu kwa nini napunguza kutoa filamu, jamani naomba niwaambie ukweli najiandaa
kupumzika kuigiza,” aliandika JB kupitia instagram yake. “Lakini najitengeneza
kuwa producer mkubwa zaidi ndiyo maana natengeneza hata tamthilia,”
Aliongeza, Nimeigiza tangu 1998 hadi sasa, nakaribia
umri wa miaka 50, kwa umri wangu natakiwa niwekeze zaidi kwa vijana ambao
naamini wanaweza kufanya vizuri zaidi. Kwa hiyo baada ya filamu ya ‘Kalambati
Lobo’ nitafanya movie yangu moja ya mwisho na baada ya hapo kazi itakayobaki ni
kuwasaidia vijana kupitia Jerusalem Film. Nawapenda sana na asanteni sana kwa
kuniunga mkono, hamjawahi kuniangusha, nawapenda sana,”
Muigizaji huyo amewai kufanya vizuri na filamu kama,
Danija, DJ Ben, Bonge la Bwana, Mzee wa Swagga pamoja na Jacob stephene,”

No comments:
Post a Comment