Ziara ya ya Snoop Dogg na Wiz Khalifa
imeendelea kukumbwa na majanga.
Jumanne hii, watu 50 wengi wao wakiwa vijana wenye umri
mdogo, walilewa chakali kiasi cha kuhatarisha maisha yao (alcohol poisoning).
Wasanii hao wapo kwenye ziara ya pamoja iitwayo The High Road Tour.
11 kati ya watu hao walilazwa kwenye hospitali za jirani
akiwemo kijana mwenye miaka 18 ambaye alianguka chini na kuvunja pua yake. Watu
kadhaa pia walishikwa kwa kukutwa na bangi kwenye show hiyo.
Vyanzo vimedai kuwa vijana hao walikuwa wakinywa vodka
zilizokuwa kwenye chupa za maji kwenye vyo na sehemu ya kuegeshea magari. Tukio
hilo limekuja siku chache tu baada ya watu 42 kuumia baada ya kuanguka kwa uzio
kwenye show yao ya Camden, NJ.

No comments:
Post a Comment