WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Amesema mtumishi yeyote
aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti anatakiwa arudi na
kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si vinginevyo.
"Tayari nimemuagiza ndugu
Zuberi Samatabu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani kuhakikisha anasimamia watumishi
wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya wilaya hiyo waishi Kibiti na si
Ikwiriri," amesema.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu ilifuatia
taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Alvera Ndabagoye
ambaye alimueleza Waziri Mkuu kuwa ni watumishi wanane pekee kati ya 74
waliopangiwa kufanya kazi kwenye wilaya hiyo wameripoti katika kituo cha
kazi
Ili kukabiliana na tatizo la
uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo kuzungumza na watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwenda wilayani
huko kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumatano,
Septemba 28, 2016 wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika ziara
yake ya kukagua shughuli za maendeleo,utendaji wa serikali na kutoa msimamo wa
serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku
Wakati huo huo Waziri Mkuu
amewataka madiwani wa halmashauri hiyo wawe wakali katika kusimamia miradi ya
maendeleo na kuacha tabia ya kuomba omba kwa wakuu wa idara ili kuepuka
kujishushia hadhi zao na kupelekea kuhujumiwa kwa miradi mbalimbali ya
jamii
Aidha aliwataka viongozi wa wilaya
hiyo kutengeneza mazingira ya kukaribisha wawekezaji na wahakikishe kwamba
uwekezaji utakaofanyika hausababishi migogoro ya ardhi kwa wananchi.
Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi
kuhakikisha wanapeleka watoto shule kwa maana Serikali imebeba mzigo wote wa
gharama za ada na uendeshaji wa shule hizo.
Alisisitiza kuwa njia pekee na ya
haraka kuondoa umaskini ni kusomesha watoto Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
ameagiza halmashauri zote nchini kutumia mfumo wa kieletroniki katika
ukasanyaji wa mapoto ili kuziba mianya ya uvujaji mapato haswa ya maliasili
No comments:
Post a Comment