Updates kuhusu afya
ya beki wa kati na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Rigobert
Song ambaye mwishoni mwa juma lililopita alikimbizwa hospitalini akiwa kwenye
hali mbaya baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa ndugu wa familia
yake, wamesema kuwa mchezaji huyo ameacha kutumia mashine za kupumua. Song
kwa sasa yuko nchini Ufaransa ambako amepelekwa kwa matibabu zaidi, baada ya
awali kulazwa katika hospitali kuu ya mjini Younde.
Song alianguka ghafla akiwa nyumbani kwake na kupoteza fahamu,
ambapo alilazimika kukimbizwa hospitalini, na toka wakati huo alikuwa akitumia
mashine maalumu za kupumulia.
Familia yake inasema kuwa ndugu yao sasa ametolewa kwenye chumba
cha wagonjwa mahututi na ameacha kutumia mashine za kupumulia. Wachezaji
wengi wa zamani na wa sasa wa Cameroon wameendelea kutuma salamu za pole kwa
familia yake wakimuombea apone haraka na kurejea kwenye hali ya kawaida, ambapo
madaktari wanaomtibu wamesema hali yake inaendelea kuimarika.
Songo alianza kuichezea timu yake ya taifa mara ya kwanza
September 1993 akiwa na umri wa miaka 17, wakati timu yake ilipocheza mchezo wa
kimataifa wa kirafiki na timu ya taifa ya Mexico jijini Los Angeles,
Marekani. Song ameichezea timu yake ya taifa mara 137 na pia aliwahi kuwa
beki kwa timu za ligi kuu ya Uingereza kama vile Liverpool na West Ham.
No comments:
Post a Comment