Umoja wa Vijana wa CUF (JuviCUF)
umewataka vijana wa chama hicho kutotoa ushirikiano kwenye ziara ya mwenyekiti
aliyevuliwa uongozi na Barza Kuu, Profesa Ibrahim Lipumba na baadhi ya wabunge
inayotarajiwa kuanza wiki hii mikoa ya Lindi, Mtwara na Tanga.
Wito huo ulitolewa jana na
Mwenyekiti wa Juvi-CUF, Hamidu Bobali alipokuwa anazungumza na waandishi wa
habari na kueleza kuwa ziara hiyo ina lengo la kukipasua chama hiko rasmi.
“Tunajua ziara hiyo inataka
kuongeza mpasuko ndani ya chama na mpasuko huo utawapa mwanya maadui zetu
‘kutupiku’ kisiasa,” alisema Bobali.
Bobali, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mchinga kwa tiketi ya chama hicho, alisema pamoja na harakati za
Lipumba tayari wabunge wa mikoa hiyo wapo katika kikao kuandaa mikakati ya
kuimarisha chama.
Kadhalika Bobali alifafanua kuwa
kama Jumuiya wanalaani kitendo kilichofanywa na kikundi cha vijana kilichojiita
cha Mkoa wa Dar es Salaam cha kutoa kashfa kwa viongozi wa Ukawa akiwamo
Freeman Mbowe na Julius Mtatiro.
Juvi-CUF iliwatoa hofu wananchi wa Zanzibar
kuhusu hali ya kisiasa iliyopo visiwani humo, kutokana na hatua mbalimbali za
kisheria zinazofuatwa ili kuhakikisha haki inapatikana kuhusu Uchaguzi Mkuu wa
2015.
Kuhusu sakata la akaunti ya chama
inayoingizwa fedha za ruzuku na za wabunge, alisema hakuna fedha za wabunge
zitakazoingia katika akaunti hiyo kutokana na mikataba inayosainiwa inahusu
Mbunge na Ofisi ya Bunge na siyo chama.
“Tumechukua hatua kuwaeleza benki
kuhusu akaunti kufunguliwa, suala hili linafanywa na bodi ya wadhamini inayoongozwa
na Khatau hivyo siyo suala rahisi yeye (Lipumba) akazipata,” alisema
Khatau.
No comments:
Post a Comment