Baadhi ya Maneno ya Uchungu waliyoyasema wazazi wa Aquiline: Baba: - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 20 February 2018

Baadhi ya Maneno ya Uchungu waliyoyasema wazazi wa Aquiline: Baba:

"Najua ni ngumu kukutana na aliyempiga mwanangu risasi, lakini laiti ningekutana naye kama ni kijana mwenye nguvu kunizidi nitapambana naye hata kumuuma kwa meno,”
“Kama ni mzee mwenzangu nitapambana naye hadi kifo ila kwa bahati mbaya siwezi kumpata, hivyo sina namna. Kwa kweli hiki kifo kimezima ndoto ya familia ya kuondokana na umasikini.”

"Jamani hii ni taa yangu imezimika na kuniacha gizani kwani toka nimepata taarifa za kifo chake sijaweza kula chochote. Nimekuwa kama nguruwe aliyetelekezwa porini bila msaada,
"Nilipopata taarifa za kifo cha mwanangu nilishtuka sana na kuhoji ni mwizi au nini kimetokea, lakini baadaye nikaambiwa ni Serikali imefanya mambo hayo. Imenitia uchungu sana na siwezi hata kula"
"Ni afadhali mwanagu angeugua nikamuuguza kuliko kifo cha ghafla alichokipata ambacho kimetuacha kwenye hali ambayo haitafutika mioyoni mwetu katika maisha yetu yote.
Mama Aquiline
"mauaji ya mwanangu ni ya kinyama na bora angekuwa mbuzi ningekula nyama kujifariji kuliko kwa mwanangu ambaye hakuna anayeweza kunifuta machozi,
"Mwanangu hakuwa mwanasiasa ameuawa akiwa kwenye gari akielekea kwenye shughuli zake, familia tulijinyima tukajichanga kwa kushirikiana na majirani ili asome aje atukomboe,” amesema.
“Leo nasubiria niletewe maiti kwenye jeneza. Kwa kweli imeniuma sana na kunikatisha tamaa. Naomba Serikali itende haki katika tukio hili,"
************************************
Hayo maneno hatakama una moyo mgumu namna gani lazima yakuumize. Dah inasikitisha sana. R.I.P Aquiline.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here