Aliyekuwa Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji amefunguka na kuweka wazi msimamo wake juu ya tukio la kupigwa risasi kwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha NIT Aqulina Akwilini na kusema kuwa chama chake cha CCM hakiwezi kukwepa juu hilo.
Shy-Rose Bhanji amesema kuwa kufuatia kifo hicho cha mwanafunzi huyo ambaye alipigwa risasi na jeshi la polisi Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati jeshi la polisi likiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Kinondoni na kudai kuwa suala hilo yeye linamsuta moyoni mwake.
"Serikali ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo. Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu, nimeshindwa kula na nashindwa kupata usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu wangu naomba unisaidie" alisema Shy-Rose Bhanji
No comments:
Post a Comment