Tamko la CHADEMA kuhusu Watu 40 waliokamatwa katika Maandamano - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday 22 February 2018

Tamko la CHADEMA kuhusu Watu 40 waliokamatwa katika Maandamano

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kitalishtaki Jeshi la Polisi na Serikali endapo watashindwa kutoa tamko kuhusu watu 40 waliokamatwa siku ya maandamano katika uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni.

Akizungumza jana  na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika alisema watu hao 40 walikamatwa February 16, 2018 wakati wakielekea Manispaa ya Kinondoni na miongoni mwao walikuwa ni wapita njia tu na wengine ni watoto waliochini ya miaka 18.

Mnyika alisema hadi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia wananchi hao 40, ambapo kisheria lilipaswa kutoa haki kwa wananchi hao kupata dhamana.

“Tunalitaka jeshi la Polisi kupitia IGP kutoa kauli  juu ya watu hao 40 wanaowashikilia na kuwaainisha kwa majina watu hao na kueleza taratibu za kuwapa dhamana ama iwapeleke Mahakamani.”  Alisema John Mnyika

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here