kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao. Katika kipindi cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo,
Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.
Ulinzi umeimarishwa kwenye
maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na
maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha, Jeshi la Polisi
halitasita kumuwajibisha mzazi ama mlezi yeyote atakayeshindwa
kutunza mtoto wake na kusababisha mtoto huyo kupotea au kupata madhara.
Pia tunawataka wananchi wote kuwa wepesi katika kutoa taarifa pindi
wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo
ya biashara. Simu za polisi endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112.
Vilevile, Jeshi la polisi
linawataka wananchi kuwa makini na watu wanaojipatia kipato kwa njia za utapeli
kwa kutumia simu na mitandao. Mtu yeyote asikubali kutaja taarifa
zake binafsi kwa mtu asiyemjua, mfano kutaja namba ya siri ya
akaunti anayotumia kuhifadhia pesa katika simu, ama kutuma pesa kwa mtu
ambaye huna uhakika naye.
Jeshi la Polisi
linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na
kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na
pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo
kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Tunawatakia watanzania
wote Pasaka njema.
Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment