Tarehe 08 Machi kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyinge wanachama wa
Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
- Hutoa fursa kwa Serikali, wananchi, wadau, na wanawake wenyewe Kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba inayohusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa jinsia!
- Siku ya wanawake duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kauli mbiu husika.
- Maadhimisho ya Siku ya Wanawake ya kila mwaka huelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na asasi kadha wa kadha katika kuwaendeleza wanawake na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo lakudumisha Amani, Usawa na Maendeleo.
KAULI MBIU YA MWAKA HUU
Kauli mbiu ya mwaka 2016 ni “50-50 ifikapo 2030: tuongeze jitihada”
Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa na mikakati thabiti yenye mwelekeo wa kufikia Agenda ya malengo ya millenia inayohimiza kufikia asilimia 50 -50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za maendeleo.Kuanzia mwaka 2005 Serikali ilipitisha uamuzi kuwa maadhimisho haya yafanyike kitaifa kila baada ya miaka mitano kutoa muda wa utekelezaji wa maazimio na kupima mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano.Mwaka 2015 Maadhimisho yalifanyika kitaifa mkoani Morogoro. Mwaka huu 2016 mikoa yote itaadhimisha siku hii katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment