Wenyeji wa mji mmoja
mdogo nchini Italia wamekuwa wakisheherekea kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza mjini
humo tangu miaka ya 1980.
Meya Giacomo Lombardo
anasema kuwa miaka ya nyuma Ostana ilikuwa na wenyeji 1,000 lakini idadi hiyo
ya watu imekuwa ikipungua kila kukicha hadi kufikia 85 sasa.
''Mara ya mwisho mtoto
kuzaliwa hapa ni mwisho wa mwaka wa 1987''
''Kati ya mwaka wa
1975 -1976 watoto 17 walizaliwa hapa''
Kwa sasa wenyeji wa
mji huo wa Ostana wameanza kuweka mikakati ya kuimarisha idadi ya watoto
wanaozaliwa kwa kuunda nafasi mpya za kazi.
Wazazi wa Pablo,
Silvia na Jose walikuwa wamepanga kuondoka Italia kabla ya wenyeji kuwapa
nafasi ya kuwa meneja wa uhifadhi wa misitu Ostana.
Kwa sasa wanapiga
msasa sheria itakayowaruhusu wenyeji wasilipe kodi mbali na kutoa nyumba za
bure kwa wenyeji wanaotafuta kazi.
No comments:
Post a Comment