Moja ya taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari asubuhi ya leo march 9 2016, ni pamoja na hili tukio la ajali ya magari matatu ambayo ni gari la abiria aina ya DCM, Lori la mchanga na gari lingine lililokuwa limebeba mchanga kugongana katika eneo la Tabata, Dar es salaam.
Hadi sasa hakujawa na uhakika wa taarifa za uhakika kuhusiana na chanzo cha ajali ikiwa ni pamoja na vifo na majeruhi, millardayo.com inaendelea kufuatilia undani wa tukio hili na endelea kukaa karibu ili kila litakalonifikia niweze kukusogezea.
Na hizi ni picha nne za kwanza kutokea katika eneo la tukio…..
Mashuhuda wakiangalia ajali eneo la Tabata, Dar
Garia la abiria likiwa limeharibika baada ya ajali
Hapa ni gari la abiria likiwa limeharibika baada ya ajali kutokea
No comments:
Post a Comment