Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr, John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wilayani Chato mkoani Geita |
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr,John Pombe Magufuli amezitaka kamati zote za shule kuhakikisha kuwa zinasimamia swala la nidhamu na utoro katika shule wanazoziongoza na kama kuna kamati yoyote ambayo itashindwa ni vyema ikajihuzuru mapema.
Wito huo ameutoa mapema leo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Chato mkoani Geita,katika shule ya sekondari Chato,ambapo amesema kuwa kwa kamati yoyote ambayo itashindwa kuhakikisha kuwa inadhibiti suala la nidhamu mashuleni ni vyema ikajiondoa mapema.
Rais Magufuli amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na wazazi kuhakikisha kuwa wanawafatilia watoto pindi wawapo shuleni ili kuweza kutengeneza Tanzania ya wasomi zaidi.
Aidha wananchi wilayani humo,wamemshukuru Rais Magufuli kwa ujio wake huku pia wakimpongeza kwa uchapakazi wake uliotukuka na kwamba wamemwomba kuendelea kuwaondoa watumishi wote ambao hawana maadili ya kazi.
Rais,Magufuli amewataka watanzania kuendelea kupendana na kuwa wamoja na kuachana na fujo na malumbano ambayo yanaweza kupelekea kutowesha amani ya nchi.
No comments:
Post a Comment