Alikuwa ametoa tamko lake katika hafla iliyopeperushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha MSNBC.
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali.
Lakini muda muda mfupi baadaye, alibadili msimamo wake na kusema ni wahudumu wa afya wanaosaidia wanawake kutoa mimba pekee wanaofaa kuadhibiwa.
Lakini hata baada ya kusema hivyo, alijitetea na kuongeza kuwa: “Msimamo wangu haujabadilika.”
Mgombea huyo anayeongoza katika chama cha Republican anaunga mkono kupigwa marufuku kwa utoaji mimba, lakini kwa kutegemea hali.
Utoaji mimba umekuwa halali nchini Marekani tangu 1973 kufuatia uamuzi wa kihistoria wa Mahakama ya Juu nchini humo.
- Trump aahidi kuvunja mkataba wa nyuklia
- Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
- Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump
Ni kupitia Mahakama Kuu pekee au marekebisho ya katiba ambapo uamuzi huo katika kesi ya Roe v Wade unaweza kubatilishwa na uavyaji mimba kuharamishwa.
Bw Trump, ambaye wakati mmoja alikuwa mfuasi wa chama cha Democratic, ameshutumiwa awali kwa kutetea haki za wanawake kutoa mimba.
Msimamo rasmi wa chama cha Republican ni kwamba utoaji mimba unafaa kuwa haramu.
Wanasiasawahafidhina na wanaharakati wanaochukulia utoaji mimba kuwa sawa na mauaji, hata hivyo, mara nyingi hukwepa kuwekea lawama wanawake wanaotoa mimba na badala yake kuwalaumu wanaowasaidia wanawake kutoa mimba.
Lengo kuu la hili huwa kuvutia wananchi ambao kimsingi hawawezi wakafurahia kuwaona wanawake wengi walioshika mimba kimakosa wakifungwa jela kwa kutoa mimba.
Viongozi wa chama cha Republican wameeleza wasiwasi wao kuhusu kuidhinishwa kwa Bw Trump kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu Novemba, hasa kwa sababu kura za maoni zinaonesha hapendwi sana na wapiga kura wa kike.
Bw Trump ameshutumiwa kwa kuwadhalilisha wanawake wakiwemo aliyekuwa mgombea urais Carly Fiorina na mtangazaji wa runinga Megyn Kelly.
Meneja wake, Corey Lewandowski, alikamatwa Jumanne akituhumiwa kumshambulia mwanahabari wa kike.
Bw Trump amemtetea Bw Lewandowski akisema hakutenda kosa lolote.
No comments:
Post a Comment