Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alitoa siku 90 kwa wakazi wa Dar es Salaam wawe wamehakiki silaha zao ifikapo Julai mosi, ikiwa ni miongoni mwa mikakati yake ya kupambana na uhalifu uliokithiri.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alihakiki silaha zake anazomiliki.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema wanaendelea kuwahimiza wananchi waendelee kujitokeza kuhakiki silaha zao kwa muda uliotolewa.
“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliokaidi kujitokeza kuhakiki silaha zao, baada ya siku 90 zilizopangwa kumalizika”alisema.
Wakati huohuo, Siro alisema wafanyabishara wanaouza vipuri vya magari vilivyotumika maeneo ya Kariakoo, wengi wanauza vilivyoibwa sehemu mbalimbali nchini.
“Nimeshapata mtandao mzima wasipoacha kununua vitu vya wizi tutawakamata na wale wanaojifanya madalali wao, wanashirikiana na majambazi hivyo nataka waache mara moja,” alisema.
No comments:
Post a Comment