Mji Umeweka Taa Za Barabarani Chini Kutokaka Na Watu Wengi Kuwa Busy Kutumia Simu Kuliko Kuwa Makini - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 4 May 2016

Mji Umeweka Taa Za Barabarani Chini Kutokaka Na Watu Wengi Kuwa Busy Kutumia Simu Kuliko Kuwa Makini



Watu wengi duniani, hasa vijana, wamegeuzwa watumwa na simu za mkononi na huwa vigumu sana kwao kuweka simu zao chini. Hili hufanyika hata wanapotembea barabarani na wataalamu wanaonya kwamba hilo limechangia ongezeko la ajali barabarani katika miji mingi.


Si ajabu kwamba katika mji wa Augsburg, Ujerumani wasimamizi wa baraza la jiji wameanzisha mfumo mpya wa kuweka taa za barabarani. Badala ya kuwekwa kwenye milingoti, taa hizo zinawekwa chini ili watu waweze kujua taa zikibadilika bila kuinua vichwa vyao. Tatizo hilo la watu kutumia sana simu kiasi cha kutotaka kujishughulisha na mambo mengine limepelekea kubuniwa kwa msamiati mpya ambapo waraibu wa hilo wanaitwa Masmombi.



Jina hili limetokana na jina zombi ambalo hutumiwa sana kueleza viumbe ambao hutembea bila kuwa na hiari na huwa hawazungumzi lolote. Tamaduni nyingi huamini kwamba mazombi hudhibitiwa na nguvu za kishirikina na sana huwa na miili ya watu waliofariki kisha wakafufuliwa kwa nguvu hizo za kishirikina.

Dhana hii ya zombi imeunganishwa na jina la simu za kisasa ambazo kwa Kiingereza hujulikana kama smartphone.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here