Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro Marekani - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 4 May 2016

Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro Marekani

Cruz
Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyang'anyiro cha uteuzi kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.

Alitoa tangazo lake punde tu baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho Indiana.
Cruz amewaambia wafuasi wake kuwa alifanya kila analoweza katika kampeni zake,lakini hakukuwa na njia ya yeye kuweza kusonga mbele zaidi.
Mwandishi wa BBC aliyepo katika vituo vya kupigia kura Indiana amesema wafuasi wa Cruz wamestushwa na kukatishwa tamaa.
Trump
Tangazo hilo linatoa mwanya kwa Donald Trump kupata uteuzi wa chama chake cha Republican.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here