Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka mkoani Arusha, Stoppa Rhymes, amewataka wasanii wa muziki nchini kutumia mandhari ya asili katika video zao na kuacha kutumia mandhari ya magorofa na magari ya kifahari ambayo amedai yamewachosha watanzania wengi.


Rappa huyo ambaye yupo chimbo mkoani Arusha kuandaa video zake 3 mpya, ameiambia Bongo5 kuwa ufike wakati wasanii waanze kujivunia vitu vyao vya asili.
“Unajua sisi tukiamua kitu kiwe kinakuwa, wasanii tunatakiwa tubadilike kidogo, watanzania wamechoka kuangalia video zenye magorofa na nyumba za kifahari,” alisema Stoppa. “Tuna mbuga za wanyama, tuna kila kitu, tukiweza kivitumia hivi, video zetu zitakuwa za kipekee na pia tutautangaza utalii wa nchi,”
Aliongeza, “Mimi tayari kuna kazi zangu tatu mpya nashoot Arusha, katika maeneo ambayo nahisi hakuna msanii yeyote ambaye amewahi kufanya kazi au kushoot, kwa hiyo mashabiki wasubirie kazi nzuri,”

No comments:
Post a Comment