Diamond: Nikisema nisainiwe na lebo nyingine, ntakuwa nabana riziki za wanaohitaji msaada - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 3 June 2016

Diamond: Nikisema nisainiwe na lebo nyingine, ntakuwa nabana riziki za wanaohitaji msaada

Hivi karibuni bosi wa WCB, Diamond Platnumz alitoa kauli iliyowatoa povu baadhi ya mashabiki wa muziki kwa kuitafsiri kauli hiyo kuwa anamuonea gere msanii mwenzake, Alikiba baada ya kusaini dili mpya na record label ya Sony Music.
13266700_1573434146290379_345940738_n
Akiongea kwenye kipindi cha Clouds E, kinachoruka kupitia Clouds TV, Diamond alisema, “Mungu kanisaidia nikadunduliza kupata kidogo changu hicho hicho ambacho nimekiinvest ambacho nafanyia shughuli yangu. Mimi nikasainiwe record label nyingine ni uongo ni kama naenda kubana riziki za watu wengine. Nimeshafanya nyimbo karibia na wasanii wote wa Afrika sasa hivi nina macollabo na wasanii wa Marekani.”

“Nikiwa labda nina uwezo wa kusema nimpigie fulani na fulani nikapate hiyo hela nikafanya kwanini nikasaini record label? Ni sawa sawa na kwenda kulitoa pato la Tanzania kuwapelekea watu bure ilhali tunaweza tukafanya wenyewe tukapata riziki, ni heri nikae nyumbani,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here