Filamu ya Kitanzania iitwayo Bahati imeshinda tuzo nchini Burundi.
Filamu hiyo imeshinda kwenye tuzo zilizotolewa katika tamasha la Festcab International Film [Festival].
“Bahati imeongozwa na mimi (Timoth Conrad) ambaye ndiye niliyeongoza filamu ya Dogo Masai ambayo ilishinda tuzo tatu nchini Marekani mwaka 2014, pia Single Zero ambayo ilishinda pia tuzo nchini Marekani 2015,” yamesema maelezo ya Conrad.
Daniel Nyalusi akipokea tuzo kwa niaba ya Conrad na wenzake
“Katika tuzo za FESTICAB BURUNDI Bahati imeshinda tuzo kwenye kipengele cha BEST FEATURE FILM (EAST AFRICA) ambapo ilikuwa ikichuana na filamu kutoka nchi mbalimbali Afrila Mashariki. Wahusika wakuu kwenye filamu ya Bahati ni pamoja na WASTARA JUMA, SIMON MWAPAGATA, SALMA SAID, KIMLOLA KIMLOLA, DOKII,” ameongeza.
“Tuzo zilitolewa nchini Burundi tarehe 24.06.2016 ambapo kwa bahati mbaya sikufanikiwa kwenda kuipokea moja kwa moja kwa sababu mpaka sasa nipo location natengeneza filamu nyingine, lakini kuna mtanzania (Daniel Nyalusi) aliyeniwakilisha kwa kuipokea tuzo hiyo nchini BURUNDI na hatimaye ameniletea na nimeipokea.”
No comments:
Post a Comment