Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, amezindua studio ya kisasa ya ‘Kaburu Record’ iliyogharimu Sh milioni 130.


Mmiliki wa studio hiyo iliyopo Sinza Palestina ametakiwa na mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha anakuza vipaji vya wasanii wachanga ili wafikie mafanikio.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika juzi, Hapi alisema serikali inaunga mkono uwekezaji uliofanywa na vijana ili kutoa ajira kwa vijana wengine.
“Huu ni wakati wa vijana wenye vipaji kupata ajira kupitia vipaji vyao ili wajikwamue kimaisha,” alisema Hapi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa studio hiyo, Msafiri Peter ‘Papa Misifa’, alisema:
Kwa upande wa Mkurugenzi wa studio hiyo, Msafiri Peter ‘Papa Misifa’, alisema:
“Najivunia kufanyakazi na wasanii wenye majina makubwa kwa sasa katika muziki nchini akiwemo Diamond, Rich Mavoko, Timbulo, Dayna na wengine hivyo tutaiendesha ili kutimiza malengo na mafanikio ya wasanii wanaochipukia,” alisema.

No comments:
Post a Comment