SERIKALI imewatoa hofu Watanzania wote Bara na Visiwani kuwa nchi iko salama na inaendelea kuwa salama pamoja na kuwapo kwa vitisho kwa njia ya mtandao.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni, wakati wa kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Nyimbo (CCM) aliyetaka kauli ya serikali kutokana kuwapo kwa taarifa za vitisho zinazotolewa kwenye mtandao wakati huu wa maandalizi ya sikukuu ya Idd el Fitr.
Alisema pamoja na kuwapo kwa vitendo vya kiuhalifu vinavyotokea, nchi bado iko salama na itaendelea kuwa salama kutokana na serikali kuhakikisha inadhibiti uhalifu huo.
Serikali imeendelea kusisitiza kuwa mikutano ya kisiasa itaendelea kuzuiwa hadi pale polisi watakapoona inafaa kufanyika.
No comments:
Post a Comment