Maafisa wakuu nchini Uganda wanasema kuwa walinda usalama wamekabiliana vikali na kundi moja la watu, waliokuwa wamejihami kwa silaha, waliojaribu kuvamia kituo cha polisi kilichoko katikati mwa Gulu.
Gulu ni mji ulioko kaskazini mwa Uganda.
Polisi inaamini kuwa shambulio hilo lilikuwa njama za kujaribu kumuokoa mwanasiasa mmoja wa upinzani anayezuliwa- Dan Oola Odiya.
Wanasema kuwa milio ya risasi ilidumu kwa muda wa dakika thelathini.
Taharuki ya kisiasa imetanda nchini Uganda, kufuatia matokeo tata ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.
- Juma lililopita, jeshi la Uganda liliwatia mbaroni askari thelathini na raia kadhaa, likisema kuwa walikuwa na njama ya kuunda kundi la waasi.
No comments:
Post a Comment