Raia wa Marekani, Omar Mateen, 29, ameishambulia kwa bunduki klabu ya mashoga iliyopo Orlando nchini Marekani.
Mateen, anayetokea Port St. Lucie Florida, ameua takriban watu 50 na kujeruhi wengine 53 na kushikilia mateka.
Polisi walitumia mabomu kumchanganya mtu huyo na kuwaokoa watu karibu 30 waliokuwa wameshikiliwa mateka. Mateen alipigwa risasi na polisi saa kumi na moja alfajiri baada ya tukio hilo kudumu kwa masaa matatu.
Hilo ni tukio baya zaidi la aina hiyo kuwahi kutokea Marekani. Maofisa kwenye hospitali ya Orlando wamedai vifo vinaweza kuongeza. Muda mfupi kabla ya shambulio hilo, Mateen alipiga simu 911 kuelezea utii kwa kundi la ISIS.
Baba yake Mateen, Mir Seddique, aliiambia NBC News kuwa mwanae alichukia baada ya kuwaona wanaume wawili wakipigana busu huko Miami miezi kadhaa iliyopita.
Kulikuwa na takriban watu 320 ndani ya klabu hiyo na karibu 100 walishikiliwa mateka.
No comments:
Post a Comment