Waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa ametaka vilevi vipigwe marufuku uwanjani kwenye Euro 2016 - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 13 June 2016

Waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa ametaka vilevi vipigwe marufuku uwanjani kwenye Euro 2016

Waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve amewataka waandaaji wa michuano ya bara la Ulaya ya Euro 2016 kukataza vilevi katika maeneo ya michezo.
EP-140929835
Amesema maeneo ya michezo ni nyeti wakati mechi zikichezwa na hata siku moja kabla ya michuano. Kauli hii ameitoa baada ya fujo kuibuka kutoka kwa mashabiki wa England na Russia. UEFA imezitahadharisha England na Russia huenda zikaondolewa kwenye michuano ya Euro 2016 kama vurugu zao zilizotokea kwenye mchezo wao wa ufunguzi huko Marseille zitaendelea.

vurugu
Matukio tofauti kabla na wakati wa mchezo huo wa Jumamosi wa Kundi B yanaonesha idadi kubwa ya mashabiki wamejeruhiwa huku shabiki mmoja wa England hali yake ikiwa mbaya hospitali.
vurugu-2
UEFA imeomba radhi kwa hali ya utovu wa nidhamu au vurugu zilizojitokeza kati ya Urusi na mashabiki wa waingereza huko Marseille.
“Tunavitaka vyama vyote vya soka FA pamoja na RFU kuwataka mashabiki wao kushangilia timu zao kwa nidhamu na utaratibu unaokubalika.”
“Pia tunavishukuru vyombo vya ulinzi na usalama vya Ufaransa kwa nguvu zao kutuliza na kuyaokoa mashindano kutoka kwenye changamoto hiyo.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here