Jay Moe amedai kuwa haoni tatizo kuona kuna watu wachache wanaohisi amewaangusha kwa kubadilika sana kwenye wimbo wake ‘Pesa ya Madafu’ kwasababu anaamini kama ataendelea kurap vile vile hawezi kufika popote.
Akiongea na kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka, Moe alidai kuwa kushindwa kubadilika kwa rappers wengi ni kikwazo kikubwa cha wao katika kupata mafanikio.
Amedai kuwa amefanya hip hop kwa miaka 16 bila kumlipa na hivyo haoni sababu ya kujifungia sehemu ambayo haimpi mafanikio.
“Leo wakitajwa wasanii wakali wa hip hop hata watano Jay Moe atatajwa lakini wakitajwa wasanii watano wa hip hop wenye mafanikio Jay Moe hayupo,” alisema. “Kwanini na mimi nisiwe kama Nay wa Mitego, kwanini mimi nisiwe kama AY na Profesa Jay wakati kipaji changu kinafaa niwe hivyo, zaidi ya hivyo. Wasanii wengi wa hip hop wanataka ku-maintain culture ambayo haipo tena. Wote tunakubali kuwa sasa hivi muziki biashara kwahiyo tukubali kufanya ule wa kibiashara ambao hatutokuwa na malalamiko ‘wasanii wa zamani tunabaniwa kwenye media’ sio kweli ni kwasababu hatujapeleka content ambayo media na wasikilizaji wanaitaka,” alisema rapper huyo.
Jay Moe amesema Pesa ya Madafu ni wimbo uliopokelewa kwa mtazamo chanya zaidi na ameona mabadiliko makubwa ukilinganisha na Hili Game iliyotoka kabla yake.
No comments:
Post a Comment