Baada Ya Matukio ya Polisi kuua watu atimaye Polisi watano wauawa Dallas, Marekani - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 8 July 2016

Baada Ya Matukio ya Polisi kuua watu atimaye Polisi watano wauawa Dallas, Marekani

Dallas
Maafisa watano wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.

Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha.
Msako mkali unaendelea kuwasaka washambuliaji hao, mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema.
Maafisa wengine saba wa polisi wamejeruhiwa, Bw Brown amesema.

Wawili wamefanyiwa upasuaji wa dharura na mmoja yumo katika hali mahututi.
Ufyatuaji risasi ulianza waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.
Maandamano hayo yalitokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile jimbo la Minnesota na Alton Sterling eneo la Baton Rouge jimbo la Louisiana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here