
Rapper
huyo ambaye kwa sasa ana jukumu la kuwalewa watoto wake wawili ambao mama yao
alishafariki dunia, ameonyesha kuchoshwa na kazi mbalimbali za nyumbani ambazo
analazimika kuzifanya.
“Najisikia kuoa tena,” alisema Afande. “Mara chache huamua kula
kwenye sufuria kwa sababu naishi mwenyewe hivyo napika mwenyewe, naosha vyombo
mwenyewe nk, hivyo kwasababu ya uvivu wangu katika kuosha vyombo wakati flani
huamua kula kwenye sufuria ili kuepuka kuchafua vyombo zaid pasi na ulazima,”
aliandika kupitia facebook yake.
Hivi karibuni alikaririwa na chombo kimoja cha habari akidai kwa
sasa yupo kwenye mchakato wa kumtafuta mwanamke sahihi ambaye atafanya naye
maisha.

No comments:
Post a Comment