Kwa mujibu wa Chidi Benz, watu wote walikuwa na uwezo wa kumwacha na
kumchoka katika majaribu aliyoyapitia, lakini si Mr Blue.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM
wiki iliyopita, Chidi alisema kuwa Blue ni rapper aliyemsaidia bila kuchoka na
anamchukulia kama mdogo wake special.
Amedai kuwa mara nyingi alikuwa
akikutana naye na kuanza kulia kwa jinsi alivyokuwa amedhoofika. “Ila
tukikutana naye sasa anaweza akaongea mara akaanza kulia hicho ndicho alikuwa
ananiboa,” alisema rapper huyo.
Amedai kuwa Blue alikuwa akitumia
muda mwingi kumpa ushauri bila kuchoka.
“Hata kesho he is there for me, he
is my young brother, I respect him, I salute him, I am there for him too,
whatever he needs I provide,” alisisitiza rapper huyo.
Kwa upande wa Diamond, Chidi amedai
kuwa naye amemfanyia mambo mengi makubwa ikiwemo kumlipia takriban milioni 27
kwaajili ya gharama za hospitali kumsaidia aachane na madawa ya kulevya.
“He did it like two times, three
times, mpaka akafikia time akawa anakasirika sasa ndio maana this time he is
happy, nipo hapo WCB narekodi nyimbo, he is happy.”
Chidi ameachia wimbo wake mpya
‘Chuma’ aliomshirikisha msanii wa WCB, Raymond.

No comments:
Post a Comment