Akihutubu katika kongamano kuu la
chama cha Democratic mjini Philadelphia, huku akishangiliwa na wajumbe, Rais
Obama amesema hakujawahi kuwa na mtu aliyehitimu zaidi kuongoza Marekani kuliko
Bi Clinton.
"Hakujawahi kuwa na mwanamume
au mwanamke, iwe mimi au Bill Clinton au mtu mwingine yeyote aliyekuwa
amehitimu zaidi kuwa rais kama yeye," amesema Bw Obama.
Amemsifu pia kwa kujikakamua na
kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa hilo kuteuliwa kuwa mgombea
urais wa chama kikubwa.
Amempongeza kwa kubomoa vizuizi na kuunda nafasi zaidi kwa
Wamarekani.
Amewaahidi Wamarekani kwamba Bi Clinton anatetea umoja na
maadili ya Wamarekani.
Bw Obama pia amemkosoa vikali mgombea wa chama cha Republican
Donald Trump.
Awali, Seneta wa Virginia Tim Kaine alikubali rais uteuzi wa
kuwa mgombea mwenza wa Bi Clinton.

No comments:
Post a Comment