Wizara zahaha kutafuta viwanja kujenga ofisi Dodoma - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 28 July 2016

Wizara zahaha kutafuta viwanja kujenga ofisi Dodoma

         dodoma+pix
Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA), Pascas Mulagiri amesema kumekuwepo na ongezeko la maombi ya wizara na idara mbalimbali za kupata viwanja ili kujenga ofisi zao Dodoma.


Amedai kuwa kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli kuhusu serikali kuhamia Dodoma, wizara, watumishi wa umma na taasisi za serikali zimewasilisha maombi ya kugawiwa viwanja kwaajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi zao.
Alisema watapima ardhi ya kutosha ili kuziwezesha wizara, taasisi, watumishi na watu watakaohamia mjini hapo kupata viwanja.
Pia aliongeza kuwa ofisi yake ina mpango wa mpito wa kupata makazi na kuhamasisha watu wenye nyumba mjini hapo na kuzipangisha kwa watumishi wa umma watakaohamia Dodoma .
Mulagiri alisema wameunda kamati maalum inayoratibiwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ili kukamilisha azma hiyo.

BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here